Friday, August 31, 2018

10. Ni lini na kwa njia ipi madhara ya dhambi yataondolewa?

Lakini siku ya Bwana itakuja kama mwivi; katika siku hiyo mbingu zitatoweka kama mshindo mkuu na viumbe vya asili vitaunguzwa na kufumuliwa , na nchi na kazi zilizomo ndani yake zitateketea. 2 petro 3:10

11. Je, dhambi na matokeo yake yatatokea tena?

Mnawaza nini juu ya BWANA? Yeye atakomesha kabisa; mateso hayatainuka mara ya pili. Nahum 1:9
Naye atafuta kila chozi katika macho yao, wala mauti haitakuwepo tena; wala maombolezo, wala kilio, wala maumivu ahyatakuwepo tena, kwakuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Ufunuo 21:4

Wala hapatakuwa na laana yoyote tena. Na kiti cha enzi cha Mungu na cha Mwana-Kondoo kitakuwepo ndani yake na watumwa wake watamtumikia. Ufunuo 22:3

9. Kiasi gani au kwa kiwango gani Yesu ameteseka kwa ajili ya wadhambi?

Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa kwa maovu yetu;adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake sisi tumepona, isaya 53:5

Je, kwanini Yesu aliamua kufanyika mwili?

    
Basi kwakuwa watoto wameshirki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yay ohayo, ili kwa njia ya mauti amharbu yeye aliyekuwa na nguvu za maut, yaani Ibilisi, waebrania 2:14


7. Kwanini Kristo alidhihishwa au kuja?

Nanyi mnajua ya kuwa yeye alidhihirishwa, ili aziondoe dhambi; na dhambi haimo ndani yake.
1 yohana 3:5

Ni moja wapo ya kazi ya Yesu alokuja kuifanya duniani.

6. Je, mwanadamu aweza kujiweka huru lkutoka katika utumwa wa dhambi?

Je, mkushi aweza kuibadili ngozi yake, au chui madoa-doa yake? Kama aweza ndipo na ninyi mwaweza kutenda mema , ninyi mliozoea kuteda mabaya.

Mabadiliko ya tabia yanapatikana kwa Mungu. Kujaribu kwa bidii zako kubadilika waweza jikuta unaumia bure na kukosa amani katika maisha, na utakatifu kuonekana kama mzigo kwako na watu wakuzungukao.

Je, Mungu ana matazamaje mtu anayetenda dhambi?

Maana mimi sikufurahii kufa kwake afaye, asema Bwana MUNGU; basi ghairini mkaishi Ezekiel 18:32

Je, kwanini Mungu hawaadhibu wadhambi mapema?

Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengne wanavyokudhani kukawia, bali huvumilia kwenu, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikilie toba. 2 petro 3:9

3. Je, watu wangapi wamehathiriwa na mauti itokananyo na kosa la Adamu?

Kwa hiyo,kama kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwasababu wote wmaefanya dhambi; warumi 5:12


Je, yapi ni matokeo ya mwisho ya kutenda dhambi?

Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu warumi 6:23

Halafu ile tama ikiisha kuchukua mimba huzaa dhambi na ile dhambi ikiisha kukomaa huzaa mauti yakobo 1:15

1. Dhambi ni nini?

Weng twaweza kujiuliza swali hili kuwa dhambi ni nini?
1 yohana 3:4 I nasema Kila atendaye dhambi, afanya uasi; kwa kuwa dhambi ni uasi